Please use this identifier to cite or link to this item: http://ir-library.mmust.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/2751
Full metadata record
DC FieldValueLanguage
dc.contributor.authorNEYOLE, EUNICE NAFULA-
dc.date.accessioned2024-04-11T06:25:34Z-
dc.date.available2024-04-11T06:25:34Z-
dc.date.issued2023-
dc.identifier.urihttp://ir-library.mmust.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/2751-
dc.description.abstractFasiri ya maana iliyokusudiwa ni jambo la kimsingi linalopaswa kutathminiwa na kupewa umuhimu na mtoa kauli katika mawasiliano yoyote. Ijapokuwa mwasilishaji ujumbe anapaswa kuteua mkakati unaomsaidia kuhawilisha ujumbe katika hali ya kufasirika vyema, kuelewesha maana na kuondoa utata katika mawasiliano, hali hii haijitokezi katika mkakati wa ufiche unaowasilisha ujumbe kwa njia isiyo wazi. Lengo la utafiti lilikuwa kuchunguza ufiche kama mkakati wa upole katika matumizi ya lugha ya ulumbi wa Bw. Manguliechi na mawaidha ya Bi. Msafwari. Madhumuni yalikuwa; kupambanua maumbo yanayobainisha mkakati wa ufiche, kubainisha miktadha ya matumizi ya ufiche na kutathmini sababu za matumizi ya ufiche katika matumizi ya lugha katika ulumbi wa Bw. Manguliechi na mawaidha ya Bi, Msafwari. Utafiti ulitumia muundo wa uchanganuzi kifani. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Upole iliyoasisiwa na Brown na Levinson (1978) wakaieneleza zaidi mwaka 1987. Mihimili mitatu ilitumiwa; mhimili wa uainisho wa maumbo ya ufiche, mhimili wa hali na muktadha pamoja na sababu zilizosababisha uteuzi wa mkakati wa ufiche katika mawasiliano. Utafiti ulihusisha eneo kitaaluma. Taaluma husika katika utafiti huu ilikuwa ya uchanganuzi wa matini ambapo matini katika utanzu wa mazungumzo zilichanganuliwa. Ulumbi na mawaidha yaliteuliwa kimakusudi kwa ajili ya dhima yake katika kuendeleza elimu ya kiasili kwa jamii. Umma lengwa ulikuwa utanzu wa mazungumzo. Usampulishaji wa makusudi ulifanywa kuteua ulumbi wa Bw. Manguliechi na mawaidha ya Bi. Msafwari. Data ilikusanywa kupitia mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo katika rekodi za kanda za maktaba ya Kituo cha Habari cha West FM, rekodi za mtandao za Mawaidha na Bi. Msafwari, mahojiano ya simu na Bi. Msafwari pamoja na mahojiano fuatilizi ya kundi teule. Data ilichanganuliwa kwa kutumia mbinu ya kufasili. Matokeo ya utafiti yamewasilishwa kwa njia ya maelezo ya aya na majedwali. Matokeo yalibainisha kuwa chuku, maswali ya balagha, mkazo kinzani na methali ni baadhi ya maumbo ya mkakati wa ufiche yaliyobainishwa ijapokuwa kwa miundo tofauti katika ulumbi wa Bw. Manguliechi na mawaidha ya Bi. Msafwari. Ilibainika kuwa, muktadha wa hali miongoni mwa aina nyingine za miktadha ulichangia pakubwa katika uteuzi wa mkakati wa ufiche. Miktadha ya kiisimu na kitamaduni ilidhihirisha matumizi ya ufiche kwa lengo la kuimarisha na kuendeleza elimu ya kiasili. Sababu tofauti zinazomsababisha mtoa kauli kuutumia ufiche zilidhihirika kufungamana na muktadha wa matumizi yake. Ufiche ulitumiwa kuhimiza, kushutumu, kuimarisha madai na kuelekeza uzingativu kwa neno husika. Utafiti huu unahitimisha kuwa, upambanuzi wa maana kusudiwa katika kauli zenye ufiche ni swala tata. Utafiti huu unapendekeza kuwa, upambanuzi wa vipengele vya kimuktadha utiliwe maanani na mpokea ujumbe ili kupunguza utata na kuielekeza fasiri yake kwa maana kusudiwa. Matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kuchangia upambanuzi wa mkakati wa ufiche katika lugha. Aidha, yatachangia elimu ya uchanganuzi matini katika Kiswahili na lugha za Kiafrika. Kutokana na faida ya matumizi ya ufiche, wawasilishaji ujumbe wanaweza kutumia njia hii kama mbinu ya kuwasilisha maana kuhusu masuala muhimu ya jamii kwa njia inayoacha athari kubwa, ilivyo katika ulumbi wa Bw. Manguliechi na mawaidha ya Bi. Msafwari. Aidha data iliyochunguzwa inaweza kutumiwa baadaye na wanaisimu katika isimu linganishi kwa tafiti za lugha za kiasilien_US
dc.subjectMKAKATI WA UPOLEen_US
dc.subjectMATUMIZI YA LUGHAen_US
dc.subjectMFANO WA MAWAIDHAen_US
dc.subjectBI. MSAFWARI NA ULUMBI WA BW. MANGULIECHIen_US
dc.titleUFICHE KAMA MKAKATI WA UPOLE KATIKA MATUMIZI YA LUGHA: MFANO WA MAWAIDHA YA BI. MSAFWARI NA ULUMBI WA BW. MANGULIECHIen_US
Appears in Collections:School of Education

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Neyole.pdf1.8 MBAdobe PDFView/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.